Bendera ya Tanzania imepeperushwa kwa mara nyingine tena kwenye jukwaa la muziki la kimataifa baada ya Mtanzania, Mayunga Malimi kushinda shindano la Airtel Trace Music Star lililo chini ya mtandao wa Airtel na kituo cha runinga cha Trace TV.
Mayunga akiimba kwa hisia kali kusherehekea ushindi wake
Fainali ya shindano hilo iliyodumu kwa masaa mawili, ilioneshwa Jumamosi iliyopita kupitia kituo cha runinga cha TRACE Urban ambapo washiriki wa nchi 13 walikuwa wakichuana.
Fainali ilifanyika jijini Nairobi, Kenya.
Mayunga alipewa ushindi na majaji akiwemo muimbaji wa Marekani kwenye asili ya Senegal, Akon, Devyne Stephens na muimbaji wa Ufaransa Lynnsha.
Mayunga baada ya kutangazwa mshindi
Mayunga aliwashinda wasanii wengi wawili walioingia kwenye hatua ya tatu bora ambao ni Jitey wa Nigeria na Baz kutoka Congo Brazzaville.
Mayunga akiwa haamini kama jina lake ndio limetajwa kama mshindi wa shindano hilo
Mtanzania huyo aliupokea ushindi huo kwa furaha iliyopitiliza kiasi cha kupoteza fahamu kipindi alipotangazwa ushindi.
Mayunga akiwa amepoteza fahamu kwa muda
Kutokana na ushindi huo, Mayunga alishinda mkataba wa kurekodi muziki na label ya Universal Music wenye thamani ya $500,000 ambayo ni takriban shilingi milioni 900. Mayunga ni mtoto wa mwisho kwenye familia yao yenye makazi yao mjini Morogoro.
Tazama picha zaidi za fainali hizo na ushindi wa Mayunga.
Shangwe ilitawala baada ya mshindi kutangazwa
Wasanii walimshawishi Mayunga kufanya muziki ni Chris Brown, Usher na Nuruelly
Wimbo wa ushindi
Akon akimpa Mayunga maneno ya kumpa ujasiri
Akon: Furahia kijana ni siku yako hii
Mayunga alipoteza fahamu mara baada ya kutangazwa mshindi
Mayunga aliwahi kupitia Machozi Band inayomilikiwa na Lady Jaydee
Mayunga atakuwa chini ya usimamizi wa Universal Music ukiwa ni mkataba wa kurekodi na promotion wenye thamani ya dola laki tano
0 comments:
Post a Comment